Tuesday, 22 December 2015

CASSIM MGANGA FT C.BELLA - SUBIRA

                         VERSE 1:
Wasikitika usije vunja shingo yo mama
Na huko kusononeka usije ita mapaka Leo
wakaja kukuparura,ukapoteza uzuri wako
Na ukija ukiolewa,usipendeze kwa mume wako
owohoo ayayayayayaa
Na ujichunge sana maana utajichakaza
Na ulipunje ujana maana utakuchakaza
Subiri subira yako maioo
ipo mikononi mwake mola baba
Subiri subira yako mamito
Ije mikononi mwako mafungu saba
Anayetoa ni mola pekee yeye
kwa kila goti na dua anajibu yeye

                      CHORUS:
Usijeitaka harusi kwa pupaa
Usije itaka harusi ukarudi na talaka
Usikimbilie mume ukaukondesha moyo
usikimbilie mume ukaukondesha moyo x2

                      VERSE 2:
kuwa na subira usiwe na pupa ooh
mola amekuumba na sifa kedekede
ukimwomba yeye atakusikia
jiamini mama usiwe na mapepe
ma ma mapepe ma ma mapepe
Punguza mapepe ma ma mapepe

Ya nini utungule angali mume majaliwa
Kwanini ujichoreshe,na Mali yako yaliwa
utabeba vibovu upewe maradhi
Kukimbilia mapenzi
uje upate tabu kwenye mavazi
Uyachukie mapenzi
Anayetoa ni mola pekee yeye
kwa kila goti na dua anajibu yeye

                          CHORUS:
Usije Itaka harusi kwa pupaa
Usije Itaka harusi ukarudi na talaka
Usikimbilie mume ukaukondesha moyo
Usikimbilie mume ukaukondesha moyo
Usije itaka harusi kwa pupaa
Usije itaka harusi ukarudi na talaka
Usikimbilie mume ukaukondesha moyo
Usikimbilie mume ukaukondesha moyo.

No comments:

Post a Comment